Kaka na dada

Kaka na dada waweza kukuwa warafiki karibu sana na saa zingine waweza kuwa adui kali. Vile wanaona mwingine unaweza kugeuka na kubadilika na vile wakati unapita na pia kulingana na umri ya mtoto na hatua ya maendeleo yake.

Kaka na dada waweza kugombana, kubishana na kujishtakiana. Hii tabia ni kawaida na ni njia moja ya watoto kujifunza kuishi na wengine.

Tabia hii inaweza kutokea kwa ajili ya mambo tofauti:

  • Saa zingine haiwezekani kutendea watoto wote sawa. Wazazi wanatakikana kuitikia umri, haiba na hali mahsusi ya kila mtoto.
  • Ni kawaida kwa ndugu na dada kufikiria na kutendea kwa njia tofauti. Pia saa zingine ni kawaida kwa watoto kukosana.
  • Ndugu na dada waweza kukosana na kupigana ili kuvuta nadhari ya mzazi yao.
  • Mara kwa mara watoto watakosana kama wanaona hawajatendewa sawa na wazazi wao.

Kuitikia kaka na dada

Thamini na heshimu roho, mahitaji na haki ya kila mtoto. Acha kuwatofautisha.

Uongoze uhusiano ya kuheshimiana kwa jamii kwa kukuwa na mipango kwa kila mtu kufuata kwa familia.

Kubali na toa sifa wakati watoto wanakaa na imani.

Acha kila mtoto wakati wa kufanya kile kinachompendeza.

Kuwa na matarajio ekevu juu ya masaa watoto wadogo wanaweza kucheza pamoja.

Toa wakati wa kucheza na kila mtoto peke yake na hata wakati nyingine kwa wote pamoja.

Wapatie watoto nafasi ya kusululisha matatizo yao kama unahakikisha mapigano yao yamedhibitiwa. Uliza watoto kama wanahitaji usaidizi wako kusululisha maneno yao. Jiingize kusululisha mapigano yao kama watoto wameshindwa na kuidhibiti. Usitafute mtu ya kumlaumu. Tafuta utambulizi.

Kumbusha watoto kufikiria juu ya vile watoto wengine wanasikia.

Saidia watoto kuelewa kwamba kila kitu kinatakiwa kutumiwa au kuchezewa na wengine.

Kusikiliza
Ndugu na dada
Update Required To play the media you will need to either update your browser to a recent version, enable javascript or update your Flash plugin.