Ulezi wa watoto wazazi wote wanapotumika

Kusawazisha sharti za kazi ambazo zimekuwa za mashindano pamoja na shughuli za jamaa wakati wazazi wote wawili ni wafanyakazi si jambo rahisi. Uangalifu taratibu pamoja na mpangilio kuhusu jamaa lako na mahitaji ya wanao ni vya mhimu na vyaweza kutuliza kwa kiasi msukosuko utokanao na wingi wa shuguli pamoja na maisha ya jamaa.

Kuchagua kumchungisha mtoto sehemu fulani kwa wakati wewe u kazini ni moja wapo wa vitu mhimu vya kuchunguza kwa makini. Ikiwa una watoto wachanga sana, kuchagua aina ya uchungaji utakaokufaa wewe na kumfaa pia mwanao ni mhimu zaidi. Ukiwa na watoto wenye miaka ya kwenda shuleni, watoto hao waweza kuchungwa kabla ao baada ya wakati wa shule. Panakuwa aina mbalimbali za huduma kwa watoto, na zaidi kuhusu watoto wachanga, pakiwemo jamaa pana, hali ya kuwachungisha watoto katika nyumba mahali fulani na vituo vingine vinavyohusika na huduma hizo.

Jitahidini kuchagua aina ya ulinzi wa mtoto wenu pamoja. Amueni ni nani miongoni mwenu atakayempeleka mtoto na kumrudisha kutoka shuleni au kituoni. Jadilieni muone ni nani awezaye kujitoa kwa kazi hiyo, kufuatana na ratiba ya kazi ya kila mmoja wenu. Ikiwa mzazi mmoja aweza kufanya hivyo, halafu mwingine awe radhi kugawanya mzigo, akiwashugulikia watoto na kujitoa kufanya kazi zingine za nyumbani.

Kuhudumia watoto wagonjwa yaweza kuwa fungo nzito mno wakati wazazi wote wanafanya kazi. Na ni kawaida watoto wagonjwe. Kwa hiyo, ni vyema kuwepo mtu mmoja mzima au wawili, pengine watu watu wengine wa jamaa, walio tayari wakati wote kuwahudumia hao watoto wanapogonjwa.

Wazazi wote wanapotumika kila mmoja wao anaombwa kutoa mchango wake sawasawa kwa kushugulikia watoto na kuzifanya kazi zingine nyumbani. Wazazi wote wawili hustahili kupitisha mda fulani pamoja kama wenye kuuanganishwa pamoja. Kupitisha wakati kila mtu upande wake, na kupitisha mda wote pamoja kama jamaa. Watoto wanahitaji kujisikia kwamba wako wa jamaa hilo, na kwamba wanapendwa bila shurti yoyote.

Wazazi wote wawili wakiwa wafanyakazi, kusaidiana katika kazi za nyumbani ni mhimu. Hasira hutokea ikiwa mzazi mmoja huachiwa jukumu lote kuhusu kazi za ndani. Watoto walio tayari na miaka ya kuinukia waweza kusaidia katika kazi hizo; pengine jamaa lote hujiunga kutumika pamoja kwa mda wa kutosha Jumamosi asubui, wakiachia jamaa au mtu binafsi wakati mwingine kuwa huru kwa ajili ya shuguli zao.

Katika jamaa lenye wazazi wote wawili wanakuwa wafanyakazi, kila mzazi anahitaji mda wake binafsi, wakati mwenziwe anakuwa na jukumu la kuwashugulikia watoto. Mda huu huupitisha kwa vitu anavyovipendelea au kama likizo.

Wazazi wote wawili wakiwa wanatumika, yaweza kuwa vigumu kupata mda wa kuwa pamoja kama watu wawili. Mda huo, wazazi wamoja hupenda waakilishwe na mtu mwingine wa kuchunga watoto badala yao wenyewe. Wazazi huhitaji mda wa pamoja wakijifurahisha pamoja na kuupitisha mda huo kwa shuguli zingine za watu wazima.