Uwoga na wasi wasi kwa watoto

Watoto wengi huwa na uwoga wakifikia umri fulani. Sana sana huwa wanaogopa giza, sauti kubwa, wanyama wakubwa, kupotea, umbo za kutisha na kulala pekee yao. Wakati mwingine huwa na uwonga zaidi kuwa watawapoteza moja wa wazazi wao kupitia ugonjwa au kifo.

Wasi wasi pia ni kitu cha kawaida katika hisia za watoto, hisia hizi zinaweza kuwa na uwoga zaidi kutokana na mabadiliko katika maisha ya watoto mfano,watoto huwa na wasi wasi wanapohama na kwenda nyumba mpya, wakijiunga na shule mpya au kujiunga na mchezo mpya. Wasi wasi pia huwajia wanapokosa kuelewa kinachotendeka au kinachotendekea wanao wapenda.

Wasi wasi kwa watoto hujionyesha kwa njia kadha, kwa mfano mtoto huwa na tabia ya kupigana na ndungu zake ama marafiki, kutoa ukali anapokosa anachotaka, kutaabika anopolala, kulia sana, kuwa na haya au pia kuwa na kiburi. Sababu za tabia hizi kwa watoto huwa ni ngumu kuelewa hivyo basi kuwa karibu na watoto wako, na kuwa mwangalifu mara kwa mara na kinachoendelea nao inaweza kukuwezesha kuona dalili kuwa wanakubatiwa na wasi wasi.

Jinsi ya kukabiliana na uwoga na wasi wasi kwa watoto

Usifanye matani na mambo yale watoto huogopa, japo uwoga unaweza kuonekana jambo la kipuzi lakini kwa watoto ni cha ukweli na wala sio mzaha. Jaribu kuzuia hasira au kuwatolea ukali watoto.

Tilia maanani mambo yanayofanya watoto kuwa na wasiwasi na kuwaahidi kuwa utawasaidia kusuluhisha shida hiyo.

Wape muda wa kuzoeana na hali hiyo kwani yaweza kuchukua wiki, miezi ama muda zaidi. Mazungumzo ya mara kwa mara na watoto kuhusu wasiwasi na uwoga pia inaweza kusaidia kupungunza uwoga.

Wape suluhisho ambazo ni rahisi na yakueleweka ili kusaidia kupungunza mashaka yao. Waeleze watoto mambo ambayo yalikupa uwoga na vile uliyakabili.

Epuka kuwaambia watoto kuwa wasiogope chochote ama hakuna jambo la kuwaogopesha kwa maana wanaweza kujuchukua ujumbe huu kama kwamba hujali hisia zao.

Saidia watoto kufikiri jambo ambalo linaweza kumpunguza wasiwasi, mfano, kama mtoto huogopa giza au usiku, mueleze kuhusu mataa yanayotumika kwenye giza au usiku, mchezeshe kwa kutumia doli ama vifaa vya kucheza iwe kama ‘walinzi’ na pia awe na masaa mwafaka ya kwenda kulala.

Watoto mara nyingi hawawezi keueleza hali yao ya wasiwasi, wao huwa na wakati mgumu kueleza yanayowatia wasiwasi na uwoga. Wasaidie kukabiliana na hali hii kupitia michezo. Mfano, kuiga kama daktari itasaidia mtoto kutokuwa na uwoga wa kwenda hospitali ama kumuona daktari..

Hali ya wasiwasi pia inaweza kukabiliwa kwa kuwa mwangalifu na vipindi vya televisheni wanavyotazama, hakikisha vipindi wanavyotazama zinafaa na haviwapi watoto uwoga.

Andaa watoto kwa hali inayokuja ambayo unajua itawatia wasiwasi, waeleze ni nini kitakuweko, kitakachotokea au ni wapi kwa kwenda iwapo watakuwa na wasiwasi. Mfano, mtoto anapoanza shule mpya, ni vyema umsidikize kwenda shuleni, ujue mahali darasa lake liko na choo. Uwe na mda wa kucheza nae kwenye uwanja wa kucheza wakati wa wikendi na kujadiliana mahali kwa kukutana akitoka shuleni.

Uwoga kwa mtoto hupungua wakati anapojihisi kuzoeana na hali;- hivyo basi usimlazimshe mtoto kukabiliana na hali ya uwoga ana kwa ana. Msaidie mtoto kuzoena na chanzo cha wasiwasi. Mfano: Kama mtoto huogopa mbwa kubwa, basi anza kwa kumwonyesha picha za mbwa kwenye vitabu, mnunulie mdoli aliye na umbo wa mbwa, mpitishe kwenye duka la kuuza wanyama kipenzi ama duka la kuuza mbwa na mwishowe kwa wakati unaofaa, mpe moyo wakuweza kumpapasa au kumguza mbwa mdogo mwenye uzoefu na watu.

Msifu mtoto kwa jitihada zake ya kukabiliana na uwoga au wasiwasi wake

Usionyeshe watoto kuwa wewe pia una wasiwasi kwa maana hiyo inaongeza wasiwasi kwao hata zaidi. Wakati mwingine wasi wasi wako inaweza kuzidi ule wa watoto na kuzidisha hali ya watoto kuwa mbaya zaidi. Basi ni vizuri kufikiri jinsi utakavyokabiliana na wasiwasi wako.

Wakati wa kutafuta mawaidha kutoka kwa mtaalam (Mjuzi)

Kwa vile hali ya wasi wasi huwapata sana watoto, ni vizuri wazazi kwenda kwa mtaalam kwa mawaidha iwapo wasiwasi huu utaanza kuwa na madhara kwa afya yao. Iwapo hali hii inadhiri hali ya kawaida ya mtoto na inaendelea kuwa mbaya zaidi na huoni dalili ya kuwa na nafuu, basi ni vizuri kutafuta ushauri kutoka kwa dakari wako, daktari wa watoto au mtaalam anayahusika na kushahuri watoto shuleni.